• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yapunguza bei ya Sukari na maziwa

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:15:55

    Serikali ya Kenya imetangaza kupunguza bei ya sukari na maziwa ikiwa ni jaribio la kuwapunguzia wakenya mzigo wa gharama ya maisha. Kufuatia tangazo hilo hivi sasa sukari ya kilo moja itakuwa ikiuzwa kwa shilingi 120 huku pakiti ya nusu lita ya maziwa itakuwa ikiuzwa kwa shilingi 50. Tangazo hili linakuja wakati ambapo upinzani umekuwa ukishambulia serikali kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa za kimsingi na kupelekea wakenya kushindwa kumudu maisha. Hivi sasa kilo moja ya sukari inauzwa kwa shilingi 160 huku pakiti ya nusu lita ya maziwa ikiuzwa kwa shilingi 60. Bei hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa ifikapo jumatatu wiki ijayo ikiwa ni wiki chache tu baada ya serikali kupunguza bei ya unga wa mahindi hadi shilingi 90 kwa pakiti ya kilo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako