Akitangaza bajeti ya mwaka wa 2017/2018, waziri wa fedha wa Tanzania Dk Philip Mpango amesema walifikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ambazo zimeonekana dhahiri zitawaondolea mzigo wananchi wa Tanzania. Miongoni mwa mambo mazuri ya bajeti hiyo ni kufuta ada ya kila mwaka ya leseni ya magari; kufuta ada ya ukaguzi wa viwango vya mazao ya biashara; kutoza kodi ya VAT kwa kiwango cha sifuri kwa huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi.
Pia serikali imetangaza kuwatambua rasmi wafanyabiashara ndogo wasio rasmi kama machinga, mama lishe, wauza mitumba, kutoza ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 0 badala ya asilimia 25 kwenye malighafi na vifaa vinavyoagizwa nje kwa ajili ya kuunganisha na kutengeneza vifaa ambavyo ni mahsusi kwa ajili ya matumizi ya walemavu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |