• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya sukari ya Mumias yamteua kaimu mkurugenzi mtendaji

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:16:30

    Kampuni ya sukari ya Mumias imemteua Bwana Josephat Asira kuwa kaimu mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo. Bwana Asira ambaye ni mkuu wa oparesheni katika kampuni hiyo ataendelea kushikilia nafasi hiyo hadi pale bodi ya kampuni hiyo itakapofaulu kumpata mkuu mpya baada ya kuondoka kwa Bwana Errol Johnson ambaye alijiuzulu mwezi uliopita. Taarifa hiyo inakuja wakati ambapo kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na msukosuko wa usimamizi hali ambayo imesababisha kampuni hiyo kuanza kudidimia. Wakati huo huo usimamizi wa shirika la ndege la Kenya Airways umetangaza mpango wa kupunguza hisa za zaidi ya wanahisa wadogo wadogo elfu 78 wa shirika hilo. Shirika hilo limetaja hatua hiyo kama inayolenga kuliweka sawa shirika hilo ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likipata hasara badala ya kupata faida. Pindi mpango huo utakapotekelezwa basi wanahisa hao watakuwa wakimiliki asilimi 6.7 ya hisa za shirika hilo badala ya sasa ambapo wanamiliki asilimia 43.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako