• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na viongozi wa nchi mbalimbali wanaohudhuria maonyesho ya kimataifa ya Astana

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:27:32

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mfalme Felipe VI wa Hispania, rais Emomali Rakhmon wa Tajikistan na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi ambao ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria maonyesho ya kimataifa yatakayofanyika huko Astana, Kazakhstan.

    Katika mazungumzo yake na mfalme wa Hispania, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Hispania kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande mbili ili kuwanufaisha wananchi wao. Pia amesema China inaikaribisha Hispania kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kutumia vizuri reli kati ya China na Ulaya inayoanzia Yiwu, China hadi Madrid, Hispania.

    Alipokutana na rais Emomali Rakhmon wa Tajikistan, rais Xi amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia moja" umepata mafanikio makubwa, katika siku zijazo pande mbili zitaendeleza ushirikiano mpya wa hali ya juu katika sekta mbalimbali.

    Rais Xi alipokutana na waziri mkuu wa India amesema China na India zikiwa ni nchi mbili kubwa zaidi zinazoendelea duniani, zinatakiwa kushirikiana kulinda amani na utulivu wa dunia, na kusukuma mbele maendeleo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako