• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping arudi Beijing baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini Khazakstan

    (GMT+08:00) 2017-06-10 18:58:29

    Rais Xi Jinping wa China amerudi Beijing baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini Kazakhstan na kushiriki katika Ufunguzi wa Maonesho ya kimataifa ya Astana.

    Wakati wa ziara hiyo rais Xi Jinping alikutana na rais Gurbanguly Berdymuhamedov wa Turkmenstan, ambapo rais Xi amesisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo, pande hizo mbili zinapaswa kufuatilia mawasiliano kati ya ngazi ya juu na ya ngazi mbalimbali, kutafuta njia ya kufanya uvumbuzi, kupanga kwa pamoja ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali katika kipindi kijacho. Inapaswa kuimarisha mawasiliano ya utamaduni, na kuongeza maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili.

    Naye Bw. Berdymuhamedov ameeleza kuwa, Turkmenstan inapenda kukuza mawasiliano ya ngazi ya juu kati yake na China, kupanua ushirikiano katika sekta za gesi, nishati isiyo na uchafuzi kwa mazingira, nishati na miundo mbinu ya mawasiliano na uchukuzi, na kuimarisha mawasiliano ya utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako