• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya kufuzu AFCON 2019: Mechi 7 zilipigwa Jumamosi.

    (GMT+08:00) 2017-06-12 08:38:58
    Taifa Stars usiku wa jana ililazimishwa sare ya 1-1 na Mamba wa Lesotho katika mchezo wa ufunguzi wa kundi L kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika uwanja wa Azam Complex Dar es salaam.

    Nahonda wa Stars Mbwana Samatta amesema hajafurahishwa kwa matokeo hayo hasa ikizingatia walikuwa nyumbani na kuwaahidi watanzania kufanya vyema mechi zijazo. Mechi zingine

    Timu za Guinea, Msumbiji na Afrika Kusini zimepata ushindi wa ugenini katika mechi za ufunguzi za kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika Cameroon 2019 zilizochezwa jana.

    Guinea iliwaangusha Ivory Coast mjini Bouake, Msumbiji ikawafunga Zambia mjini Ndola nayo Afrika Kusini imepata ushindi wa kwanza kabisa dhidi ya Nigeria, Mauritania pia imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Botswana, sawa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliyowafunga jirani zao, Kongo 3-1 wakati Burkina Faso wakapata ushindi wa 3-1 dhidi ya Angola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako