• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga Elgon Cup: Kenya yaizima Uganda

    (GMT+08:00) 2017-06-12 08:39:22
    Nahodha Darwin Mukidza ameongoza Kenya kuizima Uganda kwa jumla ya pointi 23-18 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya raga za kombe la Elgon mchezo uliofanyika jijini Kampala Uganda Jumamosi.

    Nyota huyu kutoka klabu ya KCB aliifungia Kenya Simbas pointi13 ikiwa ni pamoja na pointi 6 za mwisho.

    Uganda ilijitutumua na kupunguza uongozi wa pointi za Kenya hadi pointi 18-10. Baada ya mapumziko, Kenya ilirejea katika kipindi cha pili kwa kishindo, na hadi mchezo unamalizika Kenya waliibuka kidedea. Mchezo wa marudiano utafanyika Juni 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako