• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makao ya watoto ya Christ Cares yaleta tabasamu kwa watoto

    (GMT+08:00) 2017-06-12 09:52:32

    Tarehe 16 Juni ni siku ya Mtoto wa Afrika. Siku hizi ilitengwa kukumbuka maandamano ya watoto wa mtaa wa Soweto nchini Afrika Kusini yaliofanyika mwaka wa 1976. Watoto hao wa Soweto waliandamana kupinga elimu duni lakini wakauwawa na watawala wa ubaguzi wa rangi.

    Tangu wakati ule watoto barani Afrika wameendelea kuwa na sauti na wanalindwa kikatiba na serikali, Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine. Hata hivyo watoto wengi wanasalia kwenye mitaa kwa kukosa elimu au kwa kuwapoteza wazazi wao.

    Lakini mashirika binafsi na wahisani wanajitolea kuwatunza watoto na kuwapa matumaini maishani.

    Makao ya watoto ya Christ Cares Center mtaa wa Kiserian nje ya mji wa Nairobi yalianzishwa na Mama Mercy Elizabeth Mwangi ambaye anaishi hapa nao na kuwatunza kila siku.

    "Shule tulianza mwaka 2011 niko na watoto arobaini, wavulana 13 na wasichana 27 ambao wanalala hapa, na ambao tunawasaidia wakiamka asubuhi wanakunywa uji, saa nne chai na chakula cha mchana na jioni. "

    Mama Mercy aliacha kazi yake mwaka wa 1990 na tangu wakati huo amekuwa na moyo wa kusaidia watoto wasiojiweza katika jamii na pia mayatima.

    Anasema angeendelea kufanya kazi angekuwa na pesa nyingi lakini kidogo aizokuwa nazo wakati ule alitumia kununua kipande cha ardhi ambako sasa kumejengwa shule wanakosomea watoto hawa.

    "Miaka hiyo nilikuwa nakaa sana na watoto wale walikuwa wanaitwa chokora na niksaidia wengine kurudi shule na kuwalihsa mchana na kwa hivyo hii ni mazao ya ile kazi tulioanza hiyo miaka"

    Sasa ili kuwatunza watoto hawa mama Mercy anategemea wahisani ambao humpa misaada ya chakula, fedha na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku.

    Makao yake yamegawanishwa kwenye sehemu mbili. Moja ni shule wanakosomea na nyingine ni bweni ambako wanalala na kutumia huduma za maktaba.

    Wakiwa wamevalia sare za zambarau nyuso zao ni zenye tabasamu na kila mmoja wao ana ndoto za kufanikisha maishani.

    "Naitwa Janet Kamande nasoma darasa la saba, kila siku napenda somo la sayansi kwa sababu tunasoma kitu ambacho kiko karibu nasi na ningependa kuwa mwalimu"

    Na wengine wangependa kujiunga nasi katika studio kama watangazaji.

    Mama mercy mwaka huu amepeleka watoto kadhaa katika shule ya serikali ili waweze kunufaika na elimu ya bila malipo inayotolewa na serikali.

    Lakini wanaenda shule na kurejea hapa katika makao ya watoto.

    Mwaka huu maudhui ya sikukuu ya mtoto wa Afrika ya Juni 16 ni kuendeleza utunzaji, uwezeshaji na kutoa fursa sawa kwa watoto wa Afrika kati ya sasa na mwaka wa 2030.

    Mwalimu mkuu wa shule hii ya makao ya watoto bwana Victor Ouma anaona kwamba mtoto wa Afrika, ana nafasi ya kufanikisha ndoto zake zote lakini ikiwa tu atalindwa vizuri.

    "Naona inatubidi kumwangalia vizuri mtoto wa kiafrika, unaweza kupata kuna wengine wana uwezo na wengine hawana lakini nawaomba wazazi wajaribu kuwapa elimu. Kama hapa kuna vipaji vingi sana na naona watasaidia jamii katika siku za baadaye"

    Licha ya kuwaletea tabasabu watoto hawa, mama Mercy pia anakumbana na changamoto ikizingatiwa kwamba hasa serikali haitoi msaada kwake.

    "Hili eneo liko mbali na mjini na hali ya kuajiri waalimu waishi hapa ni ngumu. Na wakati mwingine mwalimu anakuja anatakaa kama miaka miwili anataka kwenda. Tena kuna wakati chakula inafifia. Ile changamoto nyingine ni kwamba katika hii kazi kuna wakati naona tungehitaji gari ya mradi kama hii ndio hata wakati tumepata chakula nyingi niweze kupelekea wengine, kuna mayatima wengi sana hapa nchini"

    Siku hadi siku watoto hawa wa makao ya makao ya Christ Cares Center wanahisi joto la upendo kutoka kwa mama Mercy ambaye kwao ni mama, bibi, baba, dada, kaka na mlezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako