• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za BRICS zaendelea kuwa injini ya ongezeko la uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-06-12 09:52:38

    Ripoti kuhusu maendeleo endelevu ya nchi za BRICS iliyoandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya benki ya maendeleo ya China na Baraza la China kwenye jumuiya ya washauri bingwa wa nchi za BRICS, imesema katika muda mrefu ujao, nchi za BRICS zitaendelea kuwa injini ya ongezeko la uchumi wa dunia.

    Ripoti imechambua mchango uliotolewa na nchi za BRICS katika uchumi wa dunia, hali ya maendeleo ya uchumi na changamoto zinazozikabili katika miaka 10 iliyopita, na pia kueleza uzoefu wa China wa kuendesha mashirika ya kifedha ya kuhimiza maendeleo, na kutoa mapendekezo kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kifedha na kubadilishana ujuzi.

    Ripoti pia imesema nchi za BRICS zinapaswa kuongeza udhibiti wa sera za ujumla, kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana katika mambo ya mitaji, raslimali, soko, teknolojia na raslimali watu, kuinua kiwango cha ushirikiano wa kibiashara na kupanua ushiriki wa kina kwenye mnyororo wa thamani duniani na kuendelea na juhudi za kukamilisha mnyororo huo, ili kusukuma mbele ukuaji wenye uwiano wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako