• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha rais Emmanuel Macron chaongoza kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge la Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-06-12 09:55:54

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa zinaonyesha kuwa muungano wa kisiasa unaoongozwa na Chama cha En Marche cha rais Emmanuel Macron umeongoza kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge uliofanyika jana.

    Takwimu zinaonyesha kuwa muungano huo umepata asilimia 31.37 ya kura na kuvizidi vyama vingine kwa kiasi kikubwa.

    Mashirika ya ukusanyaji wa maoni ya umma ya Ufaransa yamekadiria kwamba muungano unaoongozwa na Chama cha En Marche unatarajiwa kupata viti zaidi ya 400 kwenye bunge la taifa.

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya mambo ya ndani pia zinaonyesha kuwa asilimia 51.4 ya watu waliojiandikisha kupiga kura hawakupiga kura kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako