• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa China asema China ni nchi kubwa inayochangia zaidi katika kazi ya kubana matumizi ya nishati duniani kwa miaka miongo kadhaa iliyopita

    (GMT+08:00) 2017-06-12 18:01:19

    Wiki ya matangazo ya kubana matumizi ya nishati ya taifa kwa mwaka huu na shughuli ya siku ya taifa ya upunguzaji wa utoaji wa hewa ya carbon dioxide ilianza jana mjini Beijing. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhang Yong amesema kwenye sherehe ya uzinduzi kuwa, hivi sasa kiwango cha maendeleo ya uchumi wa China kutegemea matumizi ya nishati kimepungua kwa kiasi kikubwa, na katika kipindi kijacho China itaharakisha hatua ya kufanya uzalishaji kwa njia isiyochafua mazingira.

    Kubana matumizi ya nishati na kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati kunachukuliwa kama ni "nishati ya kwanza" inayozalishwa kwa kasi zaidi na kutumiwa kwa gharama ndogo zaidi na safi zaidi. Katika Wiki ya matangazo ya kubana matumizi ya nishati na shughuli ya siku ya upunguzaji wa utoaji wa kaboni dioksidi ya taifa kwa mwaka huu, China itaanzisha shughuli mbalimbali kwa kufuata kauli mbiu ya "kujiunga na shughuli za kubana matumizi ya nishati, na kunufaishwa kwa pamoja na hatua za kutochafua mazingira" na "kuendeleza viwanda kwa njia ya kupunguza utoaji wa hewa za kaboni dioksidi".

    Kati ya shughuli mbalimbali wakati wa wiki hii, wajumbe wa makampuni mbalimbali wametoa ahadi ya kubana matumizi ya nishati inachukua sehemu muhimu. Naibu meneja mkuu wa Kundi la mafuta ya petroli na viwanda vya kemikali la China Bw. Jiang Fangzheng anasema:

    "Kundi hili litatekeleza kwa makini vigezo vya kubana matumizi ya nishati ya taifa na ya mikoa mbalimbali, kukamilisha malengo ya kubana matumizi ya nishati ndani ya kundi hilo; kufanya ukarabati unaolenga kubana matumizi ya nishati; kuanzisha utaratibu wa kutoa tuzo kwa idara na wafanyakazi wanaochagia zaidi katika mambo hayo."

    Hivi sasa kiwango cha maendeleo ya uchumi wa China cha kutegemea matumizi ya nishati pia yamepungua kwa kiasi kikubwa. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhang Yong anasema:

    "Kati ya mwaka 2005 hadi 2016, China imebana matumizi ya nishati ya makaa ya mawe kwa tani bilioni 1.8, kiasi hicho ni sawa na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni dioksidi kwa tani bilioni 4, hali ambayo imeonesha kuwa kiwango cha ongezeko la uchumi cha kutegemea matumizi ya nishati kimepungua kwa kiasi kikubwa. China ni nchi kubwa inayochangia zaidi katika kubana matumizi ya nishati duniani katika kipindi hicho."

    Kwa mujibu wa Mipango ya maendeleo ya China, ifikapo mwaka 2020 matumizi ya nishati yatapungua kwa asilimia 15, na matumizi ya jumla ya nishati yatadhibitiwa kuwa chini ya kiwango cha tani bilioni 5 za makaa ya mawe kwa mwaka. Mbali na hayo, China inaimarisha utaratibu wa kutoa tathmini kuhusu malengo ya kubana matumizi ya nishati, kukamilisha sheria na kanuni kuhusu nishati na kubana matumizi ya nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako