• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya VIWANGO VYA RIBA VIMEUMIZA FAIDA YA BENKI

  (GMT+08:00) 2017-06-12 19:48:08
  Benki za kibiashara nchini Kenya zimerekodi kushuka kwa ukuaji wa faida katika miezi ya kwanza mitatu ya mwaka huu.

  Kushuka kwa kwanza kulionekana baada ya kupitishwa kwa Viwango vya Riba katika mwezi Septemba mwaka jana.

  Karibu benki zote, ila benki ya Diamond Trust Bank (DTB), ziliandikisha kushuka kwa faida ikilinganishwa na kile walikuwa wanapata kabla ya sheria ya riba kutekelezwa.

  Kwa mujibu wa ripoti ya benki ya fedha, DTB iliandikisha ongezeko la asilimia 8.8 katika mapato yake ya muhimu kwa kila hisa (EPS) na kufikia Sh6.3 katika robo ya kwanza ya mwaka wa 2017, ikilinganishwa na Sh5.8, iliyorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

  Kulingana na takwimu, benki nyingi zilirekodi kushuka kwa mapato ya riba ambayo imetokana na juu za riba katika malipo yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako