• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Luxembourg wakutana

    (GMT+08:00) 2017-06-12 21:08:35

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Luxembourg Bw. Xavier Bettel ambaye yupo ziarani nchini China.

    Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa Luxembourg ni mwenzi muhimu wa ushirikiano kwa China katika Umoja wa Ulaya. Amesema katika miaka 45 iliyopita tangu uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili, pande hizo mbili zimekuwa zikiheshimiana na kutendeana kwa usawa. China inapenda kuongeza uaminifu wa kisiasa kati yake na Lusembourg, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili, na kuimarisha mawasiliano na uratibu katika mambo ya kimataifa na ya kikanda.

    Bw. Bettel pia ameeleza matumaini yake ya kuhimiza biashara huria na kupenda kuimarisha mawasiliano kati yake na China ili kukabiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako