• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Rangaranga- Canadian Grand Prix: Lewis Hamilton ampoteza Sebastian Vettel

    (GMT+08:00) 2017-06-13 08:10:47
    Upinzani kati ya madereva wawili mmoja kutoka Mercedes na mwingine kutoka Ferrari ulikuwa ni kati ya mambo yaliyovuta hisia na macho ya watazamaji wengi katika mbio za rangaranga zilizofanyika usiku wa jana za Canadian Grand Prix huku wengi wakitaka kuona nani ataibuka mbabe.

    Muingereza Lewis Hamiliton kutoka Mercedes alimpoteza Sebastian Vettel wa Ferrari ambaye anatajwa kama mpizani wake mkubwa baada ya Hamilton kuibuka kidedea katika michuano hiyo huku akimuacha mbali Sebastian Vettel ambaye aliishia kushika nafasi ya 4 katika mbio hizo.

    Nafasi ya 2 ilishikwa na dereva mwenzake kutoka Mercedes, Valtteri Bottas huku nafasi ya 3 ikishikiliwa na Daniel Ricciardo toka Redbull. pamoja na Hamilton kushinda mashindano hayo ila Sebastian Vettel bado anaongoza msimamo wa madereva wa Formula One huku Lewis Hamilton akiwa katika nafasi ya pili,

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako