Rais John Magufuli wa Tanzania ameziagiza mamlaka husika kupitia upya na kurekebisha sheria ya madini ili kuhakikisha nchi hiyo inanufaika kutokana na rasilimali zake.
Rais Magufuli amesema hayo baada ya kupokea ripoti ya pili ya mchanga wa madini. Mwenyekiti wa Kamati maalum inayoshughulikia suala la madini ya Tanzania Bw Nehemiah Osoro amesema ripoti hiyo imeonesha kuwa kuna uganganyifu mkubwa kwenye biashara ya madini kuhusu kiasi cha dhahabu inayosafirishwa nje na pia kuna ukwepaji kodi.
Rais Magufuli pia ametoa amri kuwachunguza maofisa waliosaini makubaliano ya mauzo ya madini yaliyoisababishia nchi hasara ya mabilioni ya dola za Marekani. Watakaochunguzwa ni pamoja na mawaziri wa madini wa zamani na wanasheria waandamizi waliosaini makubaliano na makampuni ya kigeni yenye mianya ya kuiibia nchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |