• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfuko wa hifadhi za jamii wa China wadumisha faida

    (GMT+08:00) 2017-06-13 18:00:16

    Mfuko wa hifadhi za jamii wa China umeonyesha maendeleo mazuri kwa mwaka uliopita licha ya shinikizo la kushuka kwa uchumi.

    Baraza la Taifa la Mfuko wa Hifadhi za Jamii limesema, mfuko huo ulipata faida ya dola za kimarekani bilioni 4.7 kutokana na uwekezaji kwa mwaka jana.

    Mfuko huo ulianzishwa ili kusaidia idadi ya watu wazee nchini China na kuwa mkakati wa ziada wa kusaidia matumizi ya siku za baadaye ya hifadhi ya jamii.

    Vyanzo vya mapato ya mfuko huo ni pamoja na mgao unaotolewa kila mwaka na serikali kuu, michango ya watu binafsi, na mitaji inayotolewa na njia nyingine zilizoidhinishwa na baraza la serikali la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako