• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kiwanda kipya cha maziwa kunufaisha wafugaji Kenya

  (GMT+08:00) 2017-06-13 19:24:15

  Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa katika eneo la North Rift nchini Kenya wanatarajiwa kwamba mapato yao yatahimarika baada ya kufunguliwa kwa kiwanda cha maziwa cha dola milioni 400 mjini Eldoret.

  Sasa kiwanda hicho kipya kitasindika lita 300,000 za maziwa kwa siku ikilinganishwa na kile cha zamani kilichokuwa na uwezo wa lita 100,000.

  Mkurungezi wa kiwanda hicho Nixon Sigey amesema hii inatwezesha wakulima kupata shilingi bilioni 2 zaidi kila mwaka.

  Kiwanda hicho kinalenga kuzalisha maziwa aina ya UHT na yale ya unga.

  Akiongea kwenye hafla ya ufunguzi wa kiwanda hicho, naibu wa Rais William Ruto alisema kufunguliwa kwa kiwanda hicho kutahakikisha hakuna ukosefu w mara kwa mara wa maziwa dukani ama kupanda kwa bei.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako