• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yapaswa kujifunza Moyo wa pamoja wa watu wa China wa kujiendeleza

    (GMT+08:00) 2017-06-14 18:08:14

    Bw. Lovemore Chikova ni mhariri wa Gazeti la Herald ambalo linauzwa kwa wingi zaidi nchini Zimbabwe. Akiwa mhariri kwa miaka mingi, Bw. ametembelea China mara sita. Kuanzia mwezi Machi hadi Desemba mwaka 2016, alishiriki katika kongamano la tatu kwenye kituo cha Mawasiliano ya habari kati ya China na Afrika lililofanyika nchini China. Mbali na kupewa mafunzo darasani, vilevile alitembelea sehemu nyingi nchini China na kushuhudia maendeleo yaliyopatikana nchini humo.

    Ingawa Bw. Chikova amerudi Zimbabwe nusu mwaka uliopita, lakini China imemwachia kumbukumbu kubwa. Anasema:

    "China ni nchi yenye miujiza! Hivi sasa China imepata mabadiliko makubwa ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wakati nilipoitembelea miaka 10 iliyopita. Inabadilika kila mwaka, na mambo mapya pia yanajitokeza kila mwaka."

    Ingawa katika safari yake nchini China mwaka jana, Bw. Chikova alipanda treni ya mwendo kasi, kushuhudia magari yanayotumia nishati ya aina mpya, na teknolojia ya kisasa ya ndege zisizo rubani ambayo inaongoza duniani, pia alitembelea mikoa kadhaa nchini China. Lakini mambo yaliyomwachia kumbukumbu kubwa ni moyo wa pamoja wa watu wa China wa kujiendeleza. Anasema:

    "Wananchi wa China wana malengo ya pamoja ya kujiendeleza. Juhudi zao za kutimiza malengo hayo zimeniachia taswira kubwa. Kila mahali nilipotembelea watu wanajadili namna ya kujiendeleza."

    Bw. Chikova siku zote anafikiria jinsi China inavyojiendeleza kwa kasi na kuwa nchio ya pili kw anguvu ya uchumi duniani, na Zimbabwe inaweza kujifunza nini kutoka kwa China. Anasema:

    "Jambo muhimu la kwanza ni kuwa na moyo wa pamoja, kwani maendeleo hayatapatikana bila ya ushiriki wa wananchi. Pili ni hatua za utekelezaji. Kila mwaka nyaraka nyingi kuhusu maendeleo ya uchumi zinatangazwa nchini Zimbabwe, lakini ni chache kati yake zilizotekelezwa. Lakini nchini China, mipango mbalimbali ikitangazwa inatekelezwa."

    Kuanzia mwezi Aprili mwaka 2016, Bw. Chikova alianzisha mada kuhusu matukio mbalimbali kati ya Afrika na China katika Gazeti la Herald, ili kujulisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana nchini China. Hadi sasa anaandika makala mbalimbali kwa ajili ya mada hiyo. Anasema:

    "Nilikaa nchini China kwa miezi kumi na zaidi, kukaa kwangu kusingekuwa na maana yoyote kama sitaleta uzoefu wa China na mafanikio yaliyopatikana nchini humo kwa serikali na watu wa Zimbabwe."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako