• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Mauzo ya nguo zilizotengezwa kwa ajili ya mauzo ya nje imerudi tena Na Nairobi

  (GMT+08:00) 2017-06-14 20:07:38

  Mauzo ya nguo zilizotengezwa kwa ajili ya mauzo ya nje imerudi tena.

  Mauzo haya yatafanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Nairobi baada ya mauzo kama hayo kufanyika Mombasa na Nyeri.

  Mamlaka ya Kukuza sekta za Nje (EPZA) siku ya Jumanne ilitangaza uuzaji wa siku nne wa nguo za EPZ.

  Mauzo haya yatafanyika katika jengo la KICC, na itapatia wafanyabiashara na Wakenya nafasi ya kununua nguo bora kwa bei za nafuu.

  Uuzaji umefuata hatua ya serikali ya kuongeza upatikanaji wa soko la ndani kwa wakenya asilimia 40 kutoka asilimia 20 iliyo sasa.

  Hatua hii inaruhusu makampuni ya nguo kuuza asilimia 40 ya nguo wanazozalisha kwenye soko la ndani bila kulipa ushuru.

  Viwanda vya Mavazi EPZ huajiri karibu Wakenya 42,000, na kuzalisha mapato ya hadi sh bilioni 36.9 kutoka kwa nguo zilizokamilika kwa ajili ya mauzo ya nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako