• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumaini ya China kushiriki kombe la dunia yazima baada ya kutoka sare na Syria

    (GMT+08:00) 2017-06-15 09:09:32

    Matumaini ya timu ya Taifa ya China kufikia michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 yamezima baada ya kukubali goli la dakika za majeruhi na kupelekea kutoka sare dhidi ya Syria katika mchezo uliochezwa siku ya Jumanne.

    Mchezaji Ahmad Al Salih, alikuwa mwiba mkali mbele ya China baada ya kuisawazishia timu yake katika dakika za lala salama na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2.

    Syria inashika nafasi ya nne katika kundi lao, ikiwa na alama tatu nyuma ya timu ya taifa ya Uzbekistan ambao wana michezo miwili mkononi huku timu ya taifa ya Iran ikishika nafasi ya kwanza.

    Wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka wa 2022, Qatar, iliishangaza Korea Kusini kwa ushindi wao wa magoli 3-2, katika kundi hilo zinahitajika timu mbili ili kuweza kujikatia tiketi ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

    Timu ya taifa ya China inayo nolewa na Meneja, Marcello Lippi inaburuza mkia katika kundi hilo la A.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako