• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbwana Samatta na Jonas Mkude watemwa timu ya Taifa

  (GMT+08:00) 2017-06-15 09:10:36

  Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania 'Taifa Stars', Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushiriki michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini huku wachezaji muhimu wa kikosi hicho Mbwana Samatta na Jonas Mkude wakiachwa. Taifa Stars itaweka kambi kwa wiki moja Afrika Kusini kwa maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 25 mwaka huu.

  Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

  Michuano ya COSAFA, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania ni mwanachama wa CECAFA, imepata mwaliko kushiriki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako