• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Claudio Ranieri meneja mpya wa klabu ya Nantes ya Ufaransa

  (GMT+08:00) 2017-06-15 09:11:17

  Meneja wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri ni meneja mpya wa klabu ya Nantes, ya Ufaransa.

  Klabu hiyo ya Ligue 1 walipewa ruhusa maalum na wasimamizi wa Ligi Kuu ya Ufaransa kumsajili Mtaliano huyo, ikizingatiwa kwamba alitimiza umri wa juu zaidi unaoruhusiwa kwa waamuzi, ambao ni miaka 65.

  Ranieri aliwaongoza Leicester City, kujinyakulia taji la klabu bingwa ulaya msimu wa 2015 -16 na kuongeza umaarufu wa klabu hiyo.

  Lakini alipigwa kalamu mwezi Februari, ambapo klabu hiyo ilikuwa ikijikuta katika hatari ya kushushwa daraja baada ya kupoteza kwa mara tano mfululizo kwenye ligi.

  Ranieri alichukua uongozi baada ya Sergio Conceicao winga wa zamani wa kushoto wa Ureno kuondoka Nantes na kujiunga na Porto.

  Ranieri ana uzoefu wa kufanya kazi nchini ufaransa, alipoiwezesha Monaco kupandishwa daraja kujiunga na Ligue 1 mwaka 2012 -13 na kuwaongoza kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Paris St Germain msimu uliofuata kabla ya kuiaga timu hiyo.

  Nantes itakuwa timu ya 17 kwa Ranieri kama meneja kwa miaka 31 na ambapo amekuwa mkufunzi pia wa klabu kubwa zaidi za Italia isipokuwa AC Milan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako