• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tetesi za usajili siku ya Jumatano

  (GMT+08:00) 2017-06-15 09:12:32

  Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anashughulikia uwezekano wa kununua wachezaji watatu wa kimataifa wa Ufaransa, huku akijiandaa na wachezaji kadhaa kuondoka Emirates.

  Wenger anataka kuwasajili Kylian Mbappe, na Thomas Lemar, kutoka Monaco na Alexandre Lacazette, kutoka Lyon. Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema Arsenal wanaweza kumchukua Lacazette iwapo watawapa Olivier Giroud pamoja na pauni milioni 60, West Ham wanamtaka Giroud, ambaye amesema hataki kukaa benchi Emirates.

  Naye Meneja wa Everton Ronald Koeman anawanyatia wachezaji watatu- kiungo wa Ajax Davy Klaassen, Gylfi Sigurdsson, kutoka Swansea na beki Michael Keane, kutoka Burnley).

  Kadhalika West Brom wameanza mazungumzo ya kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, ambaye pia anasakwa na Aston Villa, Manchester City wako tayari kupunguza bei ya Samir Nasri ya Pauni milioni 16, kwa kuwa hakuna timu inayomuulizia. Beki wa Manchester United Chris Smalling, atauzwa, huku West Brom, West Ham na Everton wakimtaka, West Ham wako tayari kutoa pauni milioni 10, ingawa Manchester United wanataka pauni milioni 15. Manchester City wana matumaini kuwa Alexis Sanchez, hatosaini mkataba mpya Arsenal ili waweze kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 50.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako