• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cristiano Ronaldo ashtakiwa kwa kukwepa kilipa kodi Hispania

  (GMT+08:00) 2017-06-15 09:12:56

  Mamlaka nchini Hispania zitamfungulia mashtaka nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, akishutumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha dola za kimarekani milioni 16.5. Waendesha mashtaka wamedai kuwa kodi ni kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014 na inahusu mapato ya nje na uwanja na haki za picha zake

  Ikilinganishwa na ile iliyokuwa ikimkabili Lioneil Messi, Ronaldo kosa lake ni kubwa sana kwani wapelelezi wa kesi yake wanadai mshambuliaji huyo alifungua hadi kampuni kwa jina jipya ili kukwepa kulipa kodi na kiasi ambacho Ronaldo amekwepa ni mara 3 ya kile kilichomtia Lioneil Messi matatani.

  Messi kesi yake ilikuwa ni ukwepaji wa kodi kiasi cha euro 4.1m huku Cristiano Ronaldo ikiwa ni euro 16m, na Messi na baba yake walihukumiwa adhabu ya miezi 21 na faini ya euro 2m hali inayoonesha Ronaldo anaweza kukabiliwa na adhabu kubwa zaidi.

  Mwezi Desemba, nyaraka zilizovuja zilieleza kuwa Cristiano Ronaldo amekwepa kodi kutokana na kipato chake kuwekwa kwenye akaunti za nje ya Hispania. Ronaldo amekana shutuma hizo. Na msemaji wa wakala wa mchezaji huyo alisema mwezi uliopita kuwa mchezaji huyo hakuwa na chochote cha kuficha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako