• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Toyota Kenya yakanusha magari yake aina ya HINO ni ya kiwango cha chini.

  (GMT+08:00) 2017-06-15 19:04:16

  Kampuni ya kutengeneza magari ya Toyota Kenya imekanusha madai kwamba magari yake aina ya HINO ni ya kiwango cha chini.

  Hii inafutia hatua ya hivi karibuni ya baadhi ya wateja kwenda mahakamani kushataki kampuni hiyo kwamba magari wanayaonunua yanakuwa na matatizo ya kimitambo ndani ya miezi mitatu tu.

  Sasa Toyota inasema magari yake ni ya kudumu kama yanatunzwa vizuri kulingana na mapendekezo ya kampuni.

  Wateja wa mabasi ya na malori aina ya HINO FC500 waliwasilisha kesi mwezi uliopita wakiai kwamba breki, na injini za magari hayo zinaharibika haraka hata kabla ya miezi 36 iliotolewa na kampuni kufika.

  Toyota Kenya inasema licha ya kesi hiyo wateja wengi wameendelea kununua magari ya HINO ishara kwamba wana imani nayo.

  Wateja wameishtaki kampuni hiyo pamoja na shirika la ubora wa bidhaa nchini Kenya KEBS, na kesi itasikilizwa tarehe 26 Septemba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako