• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Serikali ya Kenya yaomba Umoja wa Mataifa kuisaidia kuhusu swala la miraa

  (GMT+08:00) 2017-06-15 19:24:58

  Serikali ya Kenya imeahidi kuchukua hatua kadhaa ili kusaidia sekta ya miraa ilioathiriwa na kufungwa kwa masoko ncini Uingereza.

  Waziri wa kilimo Willy Bett amewaambia wakulima wa miraa kwamba serikali imeomba Umoja wa mataifa kuingilia kati ili kuondoa miraa kwenye orodha ya madawa ya kulevya.

  Bett alisema ikiwa Umoja wa mataifa utaondoa miraa kwenye orodha hiyo basi wizara ya mambo ya kigeni itaiomba nchi zote zilizopiga marufuku kukubalia tena miraa kwa soko lake.

  Waziri huyo alisema pia serikali itaaanzisha mamlaka ya maendeleo ya miraa kwenye wizara hiyo na makau yake makuu yatakuwa mjini Maua eneo la Meru ambako kunakuzwa miraa kwa wingi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako