• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tazania: Benki za kijamii Tanzania kukaguliwa

  (GMT+08:00) 2017-06-15 19:30:23

  Serikali ya Tanzania ipo mbioni kuzifanyia tathmini Benki za Kijamii ili kuona kama ni sahihi kuendelea nazo ama kufutiwa leseni baada ya kubainika zilizo nyingi hazifanyi vizuri kwa sababu baadhi zinaanzishwa kwa mashinikizo ya kisiasa.

  Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya, muda mfupi baada ya kuzindua tawi jipya la Benki ya Posta Tanzania (TPB) lililopo ndani ya soko la kimataifa la Mwanjelwa.

  Alisema hadi sasa kuna benki za kijamii zaidi ya 10 baada ya benki moja kufutiwa leseni na sababu kubwa ya kutofanya vizuri ni kutokana na kuanzishwa huku zikiwa hazijakidhi vigezo muhimu jambo ambalo ni hatari kwa uchumi na wananchi wanaotumia benki husika.

  Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema ni vigumu kupiga vita umasikini kama watu hususani wenye malengo ya kuanzisha na kufanya biashara kuogopa kuingia mkopo na taasisi za kibenki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako