• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya Brexit kuanza rasmi jumatatu ijayo

    (GMT+08:00) 2017-06-16 09:29:21

    Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mazungumzo ya Uingereza kujitoa kwenye umoja huo Bw. Michel Barnier na waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya kujitoa umoja huo Bw. David Davis, wamekubali kuanza rasmi mazungumzo kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya jumatatu ijayo.

    Kuanzia wiki hii wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Uingereza wamekutana Brussles kujadili ratiba ya mazungumzo hayo.

    Taarifa iliyotolewa na Baraza la Ulaya imesema Umoja wa Ulaya utafanya kadri iwezavyo kufikia makubaliano na Uingereza, na kusisitiza matumaini yake kuwa Uingereza itaendelea kuwa mwenzi wake katika siku zijazo baada ya kujitoa kwenye umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako