• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Money Mayweather kuzichapa na Conor McGregor

  (GMT+08:00) 2017-06-16 09:50:59

  Gwiji wa ndondi duniani Jimmy Floyd Money Mayweather atazipiga na bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano litakalofanyika Agosti 26. Ingawa kila mwaka Mayweather amekuwa akisema anaachana na ndondi lakini linapokuja dau kubwa la ndondi huwa anakubali kurudi ulingoni.

  Pambano kati ya wawili hao limekuwa likizungumziwa sana japo kuna wakati ilionekana kama jambo hilo halitatokea lakini hatimaye muafaka umefikiwa na sasa Mayweather na McGregor watapanda ulingoni mjini Las Vegas. Mpambano huo utachezwa chini ya sheria za mchezo wa Boxer japokuwa McGregor hajawahi kupigana mchezo wa Boxer popote pale lakini yeye ni mchezaji wa ngumi za Kick Boxer tu na mchanganyiko wa martial arts.

  Pambano hilo litamfanya Mayweather kuweka mfukoni kiasi cha zaidi ya $milioni 100 lakini tayari wachambuzi wa masuala ya masumbwi wameshaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Mayweather na wengi wanaona kutokana na muda aliokaa nje anaweza kupigwa.

  Rais wa UFC Dana White, amefunguka kuhusu pambano hilo na kusema anasindwa kutabiri mshindi wa pambano hilo, lakini amesisitiza kuwa pambano hilo litakuwa kubwa na amemtaja Conor ni bondia mzuri anayeweza kupambana na mtu yoyote kutokana na umri wake kuwa mdogo tofauti na Mayweather mwenye umri wa miaka 40.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako