• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Beki Federico Allende amdunga sindano mchezaji wa timu pinzani

  (GMT+08:00) 2017-06-16 09:51:30

  Mchezaji wa Argentina amesababisha rabsha baada ya kukiri kwamba alitumia sindano kumdhuru mpinzani wake katika mechi ya kuwania kikombe siku ya Jumapili.

  Beki Federico Allende, wa klabu ya kiwango cha chini kwa michezo ya Pacifico, alijivuna kwenye mahojiano ya radio jinsi alivyotumia sindano kumdunga mara kadhaa mpizani wake wa klabu ya juu ya Estudiantes.

  Allende amesema wachezaji walihitaji kuwa werevu ili kupata ushindi.

  Rais wa shirikisho la soka la Pacifico Hector Moncada ameapa kumfukuza mchezaji huyo.

  Pacifico ilishinda mechi hiyo kwa magoli 3-2 na kuibandua Estudiantes nje ya mashindano kwa uchungu mkubwa.

  Wachezaji hao walikaribishwa nyumbani kama mashujaa katika mji mdogo wa magharibi wa Jenerali Alvear waliporudi kutoka Buenos Aires, pale mechi ilipochezwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako