• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FIFA Confederation Cup kuanza nchini Russia likiwa na sheria kali

  (GMT+08:00) 2017-06-16 09:53:35

  Michuano ya 10 ya FIFA Confederation Cup inatarajiwa kuanza ndani ya siku kadhaa zijazo nchini Russia, nchi ambayo ina kesi nyingi za ubaguzi wa rangi katika viwanja vya soka.

  Kutokana na jambo hilo, marefa watakaongoza michezo ya michuano hiyo wamepewa mamlaka ya kusimamisha na kuvunja mchezo ikiwa watathibitisha suala lolote la ubaguzi wa rangi katika michuano hiyo.

  Uamuzi huu ni moja ya sehemu ya 3 ambazo zinampa mwamuzi nguvu ya kusimamisha mchezo ama hata kuahirisha mchezo kabisa kutokana na vitendo visivyo vya kimichezo vya mashabiki.

  Chombo cha mamlaka ya juu ya soka kitaweka waangalizi wa vitendo vya kibaguzi.

  Mashindano ya mwaka 2017 ya Confederations Cup ni ya 10 tangu yalipoanza na hushirikisha bingwa wa kila bara, mshindi wa kombe la dunia na pamoja mwenyeji wa michuano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako