• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bodi ya Nafaka na mazao ya Kenya kuwauzia mahindi wanandoa pekee

  (GMT+08:00) 2017-06-16 20:06:55

  Bodi ya Nafaka na Mazao imetangaza kutowauzia mahindi watu ambao hawajaoa au kuolewa ila wanandoa pekee katika hifadhi kuu ya bodi hiyo mjini Eldoret. Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na upungufu mkubwa wa unga nchini Kenya hali ambayo imewafanya maelfu ya wakenya kufurika katika hifadhi kuu ya bodi hiyo mjini Eldoret wakitaka kununua mahindi. Serikali tayari imeruhusu bodi hiyo kuuzia wakenya binafsi mahindi ili kujisagia unga wa ugali.Inadaiwa bodi hiyo inahitaji wakenya wanaokwenda kununua mahindi yao kuwasilisha cheti cha ndoa au maelezo ya familia kutoka kwa chifu wa eneo lao. Baadhi ya wakazi mjini Eldoret wamedai watu ambao hawana cheti cha ndao walitakiwa kuandikiwa barua na chifu ikieleza idadi ya watoto walio nao.NCPB imesema hatua hiyo inalenga kuzuia wafanyabiashara tapeli ambao wanataka kununua mahindi kisha kuyauza kwa bei ya juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako