• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya dunia yazindua mashindano ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii

  (GMT+08:00) 2017-06-16 20:07:47

  Benki ya dunia imezindua shindano la kuandika katika mtandao wa kijamii aina ya blogu liitwalo Blog4Dev. Shindano hilo ambalo limezinduliwa wiki hii litawahusisha vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 28 kutoka nchi za Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi. Mjumbe wa Benki hiyo katika nchi hizo Bella Bird amesema wamehamasika kuongeza ushindani na kujumuisha nchi nyingi zaidi ili wapate vijana wa kike na kiume watakaojihusisha kikamilifu na masuala ya maendeleo katika nchi zao. Washindi wawili kutoka Tanzania wataungana na wenzao kutoka Malawi, Burundi, Somalia mjini Washington DC ambako ndio makao makuu ya Benki hiyo.Aidha washindi wengine wawili watateuliwa kufanya kazi kwa wiki mbili katika ofisi za benki hiyo katika nchi zao ambako watajifunza zaidi shughuli zinazofadhiliwa na benki hiyo katika nchi zao na kuhusu michakato ya kubuni na kutekeleza miradi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako