• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bunge laidhinisha mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa Kenya Airways

  (GMT+08:00) 2017-06-16 20:08:15

  Bunge la Kenya limeidhinisha shilingi bilioni 77.3 kama mkopo kwa shirika la ndege la Kenya Airways ikiwa ni juhudi za kulikwamua shirika hilo ambalo limekuwa likididimia. Bunge lililazimika kuidhinisha mkopo huo baada ya ombio hilo kuwasilishwa na kamati ya fedha, biashara ya bunge. Uamuzi huo unatarajiwa kulipiga jeki shirika hilo ambalo limekuwa lipata hasara badala ya faida katika siku za hivi karibuni na kupelekea wasimamizi kuanza mchakato wa kurudisha hadhi yake ambayo imekuwa ikififia. Tayari shirika hilo limewafuta baadhi ya wafanya kazi ikiwa ni sehemu ya mpango wa mageuzi yanayolenga kulifanya lianze kupata faida badala ya hasara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako