• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wazazi watakiwa kujenga msingi imara wa uchumi kwa watoto

  (GMT+08:00) 2017-06-16 20:08:34

  Wakati dunia inaadhimisha mtoto wa Afrika benki ya CRBD ya Tanzania imewataka wazazi kuwajengea watoto wao msingi imara wa uchumi wa kujitegemea kwa kuwafundisha kuweka akiba. Tayari benki hiyo imepunguza kiwango kinachohitajika kumfungulia mtoto akaunti ili kumjengea utamaduni wa kuweka akiba.Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa benki hiyo bwana Charles Kimei, benki imeamua kuchukua hatua hiyo ili kutoa fursa hiyo kwa watoto wengi zaidi kupata huduma za benki. Kufuatia tangazo hilo akaunti ya mtoto sasa inaweza kufunguliwa kwa shilingi elfu 5 badala ya elfu 20 za hapo awali.Ameongeza kuwa watoto wanahitaji elimu ya fedha itakayowasaidia kufanikisha ndoto zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako