• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama nchini Misri yatoa hukumu ya kifo kwa watu 31 waliohusika na mauaji ya mwendesha mashtaka wa zamani

    (GMT+08:00) 2017-06-17 18:54:29

    Mahakama nchini Misri Jumamosi imewahukumu kifo watu 31 kutokana na kuhusika na mauaji ya mwendesha mashitaka wa zamani wa umma Hisham Barakat.

    Watu hao walikutwa na hatia ya mauaji, kuhusishwa na kikundi cha kigaidi na kumiliki silaha.

    Barakat aliteuliwa kama mwendesha mashtaka mkuu kufuatia kupinduliwa kwa Rais Mohamed Morsi mwaka 2013. Aliuawa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari lake mjini Cairo tarehe 29 Juni mwaka 2015. Kundi la "the Giza Popular Resistance" lilidai kuhusika na shambulizi hilo. Kabla ya hapo, kundi la Ansar Beit al-Maqdis lililoko mjini Sinai ambalo ni tawi la kundi la IS lilitoa wito kuwataka wafuasi kuwashambulia mahakimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako