• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Paul Kagame wa Rwanda kugombea urais kwa mara nyingine

    (GMT+08:00) 2017-06-18 17:21:43

    Chama tawala nchini Rwanda FPR jana kimechagua mwenyekiti wake ambaye pia ni rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame kuwa mgombea atakayeshiriki kwenye uchaguzi wa rais wa awamu ijayo utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

    Rais Kagame amesema atafanya juhudi kushiriki kwenye uchaguzi huo, pia ameahidi kuleta mabadiliko kwa chama cha FPR katika muda wake ujao.

    Uchaguzi mkuu nchini Rwanda utafanyika tarehe 4 mwezi Agosti. Rais Kagame alipohojiwa na vyombo vya habari alidokeza kuwa, kama akipata ushindi tena kwenye uchaguzi huo, atastaafu baada ya kumaliza muda wake wa urais mwaka 2024.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako