• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yazitaka Eritrea na Djibouti zitulie kwenye mgogoro wa mpaka

    (GMT+08:00) 2017-06-19 09:22:02

    Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imetoa wito kwa Eritrea na Djibouti kutulia na kujizuia kwenye mgogoro wa mpaka kati ya nchi hizo mbili.

    Taarifa iliyotolewa na Ethiopia italeta ufuatiliaji kutokana na umuhimu wa bandari za Eritrea, ambazo imekuwa ikizitumia kwa muda wa zaidi miaka 20 iliyopita kuagiza na kusafirisha bidhaa zake nje.

    Hali ya wasiwasi imeibuka kwenye mpaka kati ya Djibouti na Eritrea, muda mfupi baada ya kikosi cha wanajeshi 450 kutoka Qatar kuondoka ghafla. Mwaka 2008 mgogoro wa mpaka kati ya nchi hizo mbili ulisababisha vifo vya watu kadhaa kutoka kwa pande zote, na vikosi vya Qatar vililetwa kulinda utulivu kwenye eneo hilo.

    Ethiopia inaona njia yake kuelekea bandari za Djibouti ni suala la usalama wa taifa, kwa kuwa asilimia 95 ya biashara na nje inafanyika kupitia bandari za Djibouti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako