• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka la Wanawake Tanzania: Uchaguzi kufanyika Julai 8.

  (GMT+08:00) 2017-06-19 09:34:41

  Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), kimetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa leo, na mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni.

  Mushumba amesema kwamba nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako