• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndondi: Mayweather kuzichapa na Mcgregor mwezi Agosti

  (GMT+08:00) 2017-06-19 09:49:25

  Bingwa wa zamani wa ngumi za kulipwa, Floyd Mayweather atarejea tena ulingoni kupigana na mbabe Conor Mcgregor kwenye pambano la uzani wa kati litakalopigwa huko Las Vegas tarehe 26 mwezi August.

  Nyota hao wamethibitisha kuwepo kwa pambano hilo kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo Mayweather ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba ni rasmi sasa kwamba pambano hilo lipo huku Mcgregor naye akisema kuwa pambano limepamba moto.

  Pambano hilo limepewa jina la "The Money Fight" ikimaanisha kuwa ni pambano la fedha nyingi kwani kila mmoja atajinyakulia kitita cha dola milioni 100 kwa kukubali kucheza pamabano hilo, ikiwa ni kando ya fedha atakayokabidhiwa mshindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako