• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Kenya yawakamata watuhumiwa 88 wa kigaidi

    (GMT+08:00) 2017-06-19 18:54:49

    Polisi nchini Kenya leo imesema imewakamata watu 88 wanaotuhumiwa kuwa magaidi mjini Nairobi kwa kupanga kufanya mashambulizi wakati wa kusherehekea kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

    Ripoti iliyotolewa na polisi imesema, watuhumiwa hao wakiwemo raia 15 wa kigeni 15 na wakenya 73 walikamatwa alhamis iliyopita kwenye kituo kimoja kilichopo eneo la makazi la Eastleigh huko Nairobi lenye raia wengi kutoka Somalia.

    Polisi walisema kuwa operesheni ya ushirikiano kati ya kikosi cha kupambana na ugaidi, kikosi cha anga na idara ya upelelezi ilivamia kituo hicho baada ya kupata taarifa za kipelelezi kuwa kuna watu wanaoshukiwa kuwa na msimamo mkali na wanaofanya biashara haramu ya kusafirisha watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako