• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya Brexit yaanza rasmi Brussels

    (GMT+08:00) 2017-06-20 10:15:27

    Mazungumzo kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya yameanza rasmi mjini Brussles, ambapo wajumbe wa pande mbili wamethibitisha kuwa zitaweka mkazo kwenye masuala ya malipo ya Uingereza ya kujitoa Umoja wa Ulaya na uhakikisho wa maslahi ya raia wa Uingereza na wa nchi za Umoja wa Ulaya wanaoishi katika upande mwingine.

    Mjumbe mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw Michele Barnier amesema Umoja wa Ulaya unapenda kushirikiana na Uingereza badala ya kupingana nayo. Kwa upande wake mjumbe wa Uingereza Bw David Davies amesema ana imani ya kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya.

    Katika siku ya kwanza ya mazungumzo, pande mbili zimekubali kuunda timu tatu zitakazoshughulikia masuala ya kifedha, haki za kiraia na masuala ya kisheria mtawalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako