• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madagascar yapokea tani zaidi elfu 4 ya msaada wa chakula kutoka China

    (GMT+08:00) 2017-06-20 10:26:17

    Rais Hery Rajaonarimampianina wa Madagascar jana katika bandari ya Tamatave alipokea zaidi ya tani elfu 4 za msaada wa chakula uliotolewa na serikali ya China.

    Msaada huo umekaribishwa kama ni utekelezaji wa makubaliano kati ya serikali ya China na Madagascar yaliyosainiwa tarehe 27 Machi wakati rais wa Madagascar alipofanya ziara nchini China.

    Rais Rajaonarimampianina amesema miezi miwili tu baada ya kukutana na rais Xi Jinping wa China Madagascar imeona hatua halisi ya China kutekeleza ahadi yake, kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya waathiriwa wa maafa ya ukame na kimbunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako