• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali na waasi nchini Afrika ya Kati wasaini makubaliano ya amani mjini Rome

    (GMT+08:00) 2017-06-20 10:26:42

    Makubaliano ya amani yamesainiwa mjini Rome kati ya serikali ya jamhuri ya Afrika ya Kati na kundi la waasi.

    Makubaliano yaliyofanikishwa na taasisi moja ya kidini na jumuiya ya kimataifa yanatarajiwa kukomesha vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo iliyoanza mwaka 2012.

    Makubaliano hayo yanatoa wito wa kusimamisha vita mara moja, kuanzisha kikosi cha kulinda utulivu wa taifa, kuondoa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya viongozi wa Afrika ya Kati, kuhakikisha misaada ya kibinadamu inasafirishwa bila vikwazo, na kuwarejesha wakimbizi nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako