• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia na Rwanda zasaini makubaliano ya kuboresha ushirikiano

    (GMT+08:00) 2017-06-20 19:12:59

    Zambia na Rwanda zimesaini nyaraka tatu za makubaliano yanayolenga kuimarisha ushirikiano baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa nchi hizo yaliyofanyika mjini Lusaka, Zambia.

    Makubaliano hayo yamesainiwa baada ya mazungumzo kati ya rais Paul Kagame wa Rwanda aliyeko ziarani nchini Zambia na mwenyeji wake Edgar Lungu wa Zambia. Makubaliano hayo ni pamoja na huduma za usafiri wa anga, ulinzi, na usalama, na pia kubadilishana wafungwa.

    Rais Lungu amesema ziara ya rais Kagame inaashiria hatua kubwa katika kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kwamba Zambia iko tayari kujifunza kutoka Rwanda mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini humo katika kilimo na usalama wa chakula.

    Kwa upande wake, rais Kagame amesema ziara yake ni muhimu kwa kuwa itasaidia kuongeza ushirikiano wa kina unaolenga kuboresha maisha ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako