• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul yaendelea polepole

    (GMT+08:00) 2017-06-21 09:55:58

    Jeshi la serikali la Iraq linaendelea kupambana na kundi la Islamic State kwenye ngome yake ya mwisho magharibi mwa Mosul, lakini mapambano hayo yanaendelea polepole.

    Ofisa mmoja wa jeshi la Iraq amesema walipata upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa kundi hilo, ambao wametega mabomu mengi na kupanga wadunguaji kwenye majengo na barabara, na kupunguza kasi ya jeshi la serikali kusonga mbele.

    Habari pia zinasema, gari moja la waandishi wa habari lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini magharibi mwa Mosul, na kusababisha vifo vya wanahabari wawili wa Iraq na Ufaransa, na wengine wawili walijeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako