• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miundo mbinu na masoko zitasaidia Afrika kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2017-06-21 10:14:58

    Utafiti wa benki ya dunia mwaka 2015 unaonyesha kwamba nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ndio zenye uchuumi unokua kwa haraka zaidi.

    Tangu mwaka wa 2010 Jumuiya hiyo imepiga hatua kadhaa za kuendeleza uchumi wake kama vile kuwa na soko la pamoja na mpango wa kuwa na sarafu moja ulioanzishwa mwaka 2013. Na tangu mwaka 2,000 Jumuiya hiyo imevutia uwekezaji wa moja kwa moja wa zaidi ya dola bilioni 28.

    Hata hivyo baadhi ya wakaazi wake zaidi ya milioni 173,500,000 bado wanakabiliwa na umaskini.

    Mkurungezi wa shirika la kiuchumi la kikanda bwana James Shikwati kuhusu swala hilo la upunguzaji wa umsakini amesema, kupunguza umaskini huwa ni jambo ambalo linahitaji wananchi wote kutia bidii na pia linahitaji serikali kuwezesha masoko. Ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki ziandae wananchi wake waweze kuchukua fursa ya pendekezo la "Ukanda mmoja na Njia moja" kuuza bidhaa zao, na kuweza kupata urahisi wa kubadilishana mawazo. Ameongeza kuwa, Kenya inapaswa kuchurua fursa hii, na kuimarisha ushirikiao na nchi wanaoshiriki kwenye pendekezo hilo katika sekta za biashara na ujenzi wa miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako