• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Russia

    (GMT+08:00) 2017-06-21 10:31:01

    Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya watu binafsi na mashirika 38 ya Russia ili kujibu vitendo vya Russia kuhusu suala la Ukraine.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema vikwazo hivyo vipya vinalenga kuadhibu vitendo vya kukwepa vikwazo vilivyopo, na kusawazisha vikwazo vya Marekani na nchi washirika wake.

    Kwa mujibu wa vikwazo vipya, mali za watu binafsi na mashirika hayo zilizomo Marekani zitazuiliwa, na wananchi wa Marekani watapigwa marufuku kufanya biashara nao.

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw Steven Mnuchin ametoa taarifa akisema serikali ya Marekani imefanya juhudi kulinda mamlaka ya Ukraine kwa njia ya kidiplomasia, na vikwazo vipya vina lengo la kuongeza shinikizo dhidi ya Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako