• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika wachangia maendeleo ya uchumi na biashara katika nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-21 16:56:05

    Ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa makubaliano ya Mkutano wa viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2006, mfuko wa maendeleo ya China na Afrika unaoshughulikia mambo ya Afrika ulizinduliwa tarehe 26 Juni mwaka 2007. Wakati maadhimisho ya miaka 10 tangu kuzinduliwa kwa mfuko huo yanapokaribia, mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo Bw. Chi Jianxin amehojiwa na mwandishi wa habari wa Radio China Kimataifa. Katika mahojiano hayo, kwanza Bw. Chi Jianxin amefurahia juhudi za mfuko huo katika kuelekeza na kuunga mkono u viwanda vya China kuongeza uwekezaji barani Afrika katika miaka 10 iliyopita, na kuchangia kuhimiza maendeleo ya uchumi barani Afrika. Anasema:

    "Tumehimiza viwanda vingi vya China kuwekeza barani Afrika, na kuongeza ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika, na kuhimiza ushirikiano kati ya Afrika na nchi nyingine duniani. Wakati huo huo ushirikiano wa uwekezaji huo umechangia maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika, kuongeza mapato ya kodi na uuzaji bidhaa nje, utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii za huko, ni pia kuinua uwezo wa nchi za Afrika wa kupata maendeleo endelevu ya uchumi na jamii."

    Kama Bw. Chi alivyosema, katika muda wa miaka 10 iliyopita mfuko wa China na Afrika unaunga mkono viwanda vya China kufanya ushirikiano na nchi za Afrika, na kupata matokeo mazuri katika kuhimiza mchakato wa viwanda barani Afrika. Takwimu zinaonesha kuwa, tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika imeongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 2.56 za mwaka 2006 hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 34.7 za mwaka 2015. Hadi sasa, thamani ya uwekezaji wa mfuko huo katika miradi 90 ya nchi 36 barani Afrika imezidi dola za kimarekani bilioni 4.3, ambapo miradi ya uwekezaji inahusisha ushirikiano wa nishati, ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maisha ya wananchi.

    Bw. Chi Jianxin pia amesisitiza kuwa, uwekezaji wa mfuko huo katika ujenzi wa nchi za Afrika ni wa kibiashara, na unazisaidia zaidi nchi za Afrika kujiendeleza. Bw. Chi anasema:

    "Fedha za Mfuko wa maendeleo ya China na Afrika zinatumiwa kama ni uwekezaji, wala si misaada au mikopo. Uwekezaji kama huo hautaleta mizigo kwa sehemu za huko, lakini faida halisi itapatikana katika sehemu zinazowekezwa. Viwanda kama hivyo vitaleta faida katika utoaji wa nafasi za ajira, mapato ya kodi na viwanda vinavyohusika, na kuchangia kuleta maendeleo endelevu ya uchumi wa huko."

    Tangu rais Xi Jinping wa China alipotoa pendekezo la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda mmoja, njia moja" mwaka 2013, utekelezaji wa pendekezo hilo umehusisha mabara ya Asia, Ulaya ya Afrika. Kuna uelewa mbaya kuhusu pendekezo hilo, kuwa litapunguza hadhi ya Afrika katika ushirikiano kati ya China na nchi nyingine duniani. Akizungumzia suala hilo, Bw. Chi anasema:

    "Pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja' linafungua mlango kwa nchi zote duniani, hivyo ushirikiano kati ya China na Afrika unaweza kunufaishwa kutokana na pendekezo hilo. Mipango iliyotolewa na rais Xi Jinping kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika, pamoja na ushirikiano wa nishati kati ya pande hizo mbili, na hatua ya kuhimiza viwanda vya utengenezaji wa vifaa kuanzisha biashara katika nchi za nje, vyote vinalingana na kanuni ya pendekezo hilo. Hivyo maendeleo ya utekelezaji wa pendekezo hilo yatahimiza bidhaa za nchi za Afrika kuuzwa katika nchi zilizoko katika kanda ya 'Ukanda mmoja, Njia moja', na pia kuchangia kupanua soko kwa nchi za Afrika."

    Bw. Chi Jianxin ana imani kubwa na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika siku za baadaye, akisema katika kipindi kijacho, mfuko huo utafuata hali halisi ya nchi tofauti za Afrika, na kutafuta njia mpya za ushirikiano katika sekta muhimu zikiwemo ujenzi wa miundo mbinu na viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako