• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia kujibu hatua ya Marekani kuiwekea vizuizi nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2017-06-21 17:57:08

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Ryabkov amesema nchi hiyo itachukua hatua kujibu vizuizi vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo kutokana na msimamo wa Russia kuhusu suala la Ukraine.

    Bw. Ryabkov amesema hayo alipohojiwa na shirika la habari la Russia Russia Today. Amesema Russia inasikitishwa na uamuzi wa Marekani wa kuongeza vizuizi dhidi yake, na kwamba Marekani imekwenda kinyume na taarifa ya zamani ya kutarajia kuboresha uhusiano na Russia. Amesema Marekani imeacha tena fursa ya kuboresha uhusiano huo, hivyo Russia itachukua hatua kujibu jambo hilo, na sera za Russia hazitabadilika kutokana na vizuizi hivi.

    Jana, Marekani ilitangaza kuweka vikwazo dhidi ya mashirika na watu wengi wa Russia akiwemo naibu waziri wa maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, Sergei Nazarov.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako